Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limetoa wito kwa wasanii na wadau wa sanaa wanne kufika katika afisi zake leo, Septemba 22, 2026, zaa nane unusu, kwa ajili ya mahojiano.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na BASATA kupitia ukurasa wake wa Instagram, wasanii hao ni wanamuziki Nandy na Harmonize, Director Kenny na Millen Hapiness Magese.
BASATA ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, inayosimamia na kuendeleza sekta ya sanaa nchini Tanzania.
Mara nyingi wasanii wakialikwa kwa namna hii, huwa ni kwa sababu ya kukiuka maadili, isijulikane walichofanya Harmonize, Director Kenny na Hapiness.
Kwa upande wa Nandy, inaaminika kwamba ameitwa kutokana na vazi aliloonekana nalo jukwaani katika uzinduzi wa mashindano ya ulimbwende ya Miss Universe Tanzania, hivi maajuzi ambalo lilikuwa limenata mwili wake na kuonyesha umbo lake.
Msanii huyo anajiandaa pia kwa tamasha yake ijayo Septemba 26, 2026, katika eneo la Dar Village, anapoadhimisha miaka 10 katika tasnia ya muziki.