Nyota wa muziki nchini Tanzania Zuchu, anaendelea kupokea wageni katika chumba chake cha hospitali baada ya kujifungua, mgeni wa hivi punde akiwa mkewe Rais.
Alitembelewa na mke wa Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi aitwaye Mariam Mwinyi, leo tarehe 03 Agosti 2026.
Zuchu mzaliwa wa Zanzibar lakini anayeishi Dar es Salaam alijifungua mtoto wa kike juzi na amekuwa akitembelewa na wengi hospitalini baada ya kupata salama.
Mama Mariam alifika huko akiwa na lengo moja tu, kumulia msanii Zuhura Othman Soud maarufu kama Zuchu hali baada ya kujifungua mtoto wa kike na Naseeb Abdul almaarufu Diamond juzi tarehe 01 Agosti 2026 katika Hospitali ya Saifee, iliyopo Kata ya Kinondoni Mtaa wa Ada, Jijini Dar es Salaam.
Mama Mariam Mwinyi amempongeza kwa kujifungua salama na kuwatakia kheri yeye pamoja na mtoto wao afya njema, maisha marefu yenye baraka na mafanikio.
Kwa upande wao, Zuchu na Diamond wamemshukuru Mama Mariam Mwinyi kwa kutenga muda wa kufika kuwajulia hali na kuwatembelea wakieleza kuwa hatua hiyo ni faraja kubwa kwao na kwa familia katika kipindi hiki muhimu.