Eddy Kenzo na mkewe wajaliwa mtoto

Sasa wana watoto wawili pamoja lakini Kenzo ana jumla ya watoto wanne.

Marion Bosire
1 Min Read
Eddy Kenzo

Mwanamuziki wa Uganda Eddy Kenzo na mkewe ambaye ni mbunge Phiona Nyamutooro wamebarikiwa na mtoto wa kike huku familia yao changa ikizidi kukua.

Habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo zilisambaa leo asubuhi huku wengi wakitumia mitandao ya kijamii kupongeza wanandoa hao.

Mtoto huyo wa kike anakuwa mtoto wa pili wa wanandoa hao kwa pamoja, mtoto wao wa kwanza akizaliwa hata kabla ya wawili hao kufunga ndoa yao rasmi.

Kwa nyongeza hiyo ya hivi karibuni, Eddy Kenzo sasa ana watoto wanne wanaojulikana hadharani. Ana watoto wawili na Mheshimiwa Nyamutooro (mvulana na msichana), binti mmoja Amaal Musuuza na mwimbaji Rema Namakula na mtoto mwingine Maya Musuuza kutoka kwenye uhusiano wa awali na Tracy Nabatanzi.

Inaarifiwa kwamba mama na mtoto mchanga wako katika hali nzuri huku Jina la mtoto huyo wa kike likiwa bado halijatangazwa, lakini maelezo zaidi yanatarajiwa kutolewa na familia katika siku zijazo.

Kenzo na Phiona walifanya harusi ya kitamaduni Jumamosi, Juni 29, 2024 hafla ambayo ilistahili kuwa ya kwanza huku harusi ya kanisani ikipangwa.

Share This Article