Kamati ya elimu ya bunge yaongeza muda wa umma kutoa maoni

Miswada hiyo sita inalenga kuleta mabadiliko kadhaa katika elimu ya msingi,utathmini wa mafunzo ya Walimu,uhutimu wao pamoja na ufadhili wa elimu ya vyuoni.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kamati ya kitaifa ya bunge kuhusu elimu imeongeza muda kupokea maoni ya umma  kuhusu miswada sita ya mabadiliko katika sekta ya elimu iliyopendekezwa .

Zoezi la kuchukua maoni kutoka kwa umma lilipaswa kufungwa mwishoni mwa juma hili lakini sasa litakamilika Oktoba 2 mwaka huu .

Zaidi ya kaunti 16 zikiwemo West Pokot, Marsabit, Mandera, Nandi, Bungoma, Garissa, Busia, Lamu, Vihiga, Kitui, Siaya, Migori, Tharaka-Nithi, Nyamira, Bomet na Samburu zinatarajjiwa kurtoa maoni yao katika kipindi kilichosalia.

Kaunti zote 47 zinatarajiwa kutoa maoni kufikia mwishoni mwa zoezi hilo lililoanza tarehe 14 mwezi huu.

Chama cha walimu wa shule za sekondari nchini (KUPPET) kilitaka kusimamishwa kwa zoezi hilo kikihoji kuwa muda huo uliopendekezwa ulikuwa mfupi.

Kaunti hizo 16 zilikuwa zimeachwa nje ya zoezi hilo awali.

Miswada hiyo sita inalenga kuleta mabadiliko kadhaa katika elimu ya msingi,utathmini wa mafunzo ya Walimu,uhutimu wao pamoja na ufadhili wa elimu ya vyuoni.

Share This Article