Hali ya suitafahamu ingali inaghubika soka ya Kenya huku tarehe mpya ya kuanza kwa msimu wa mwaka 2026/2027 ikiwa haijulikani.
Akiwahutubia Wanahabari Jumatatu Rais wa FKF Hussein Mohammed, alitaka kutolewa kwa agizo mbili zinazokinzana kutokana kwa Mahakama zimeibua mkanganyiko mkubwa ligini.
Agizo la Mahakama Kuu ya Murang’a a Septemba 18, lilisimamisha kuanza kwa msimu wa Ligi kuu hadi pale mechi ya mchujo baina ya Kariobangi Sharks na Mombasa United itakapochezwa.
Siku moja baadaye Mahakama Kuu ya Kiambu ilitoa agizo kwa FKF kutoa ratiba ya mechi za msimu huu ikijumuisha klabu ya Mombasa United bila kuchezwa kwa mechi ya mchujo.
Hussein aidha,ameelekezea kidole cha lawama kwa baadhi ya viongozi wa soka humu nchini wanaojumu mchezo kupitia kwa siasa dunia za kibinafsi.
Ligi hiyo ilitahili kuanza rasmi Jumamosi iliyopita lakini ikasitishwa tena kutokana na agizo la Mahakama.
aliongeza kuwa shirikisho linajadiliana na pande husika ili kupata mwafaka kuhusu mustakabali wa ligi kuu msimu huu.