Serikali kufanya kazi na Wakenya wanaoishi ughaibuni kukuza maendeleo

Rais William Ruto alisema hayo alipokutana na Wakenya wanaoishi nchini Marekani kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Martin Mwanje
1 Min Read
Serikali ya Kenya Kwanza imeahidi kufanya kazi na Wakenya wanaoishi ughaibuni kuendeleza ukuaji jumuishi na maendeleo ya kitaifa. 
Rais William Ruto alitoa ahadi hiyo alipokutana na Wakenya wanaoishi nchini Marekani jijini New York kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 
Mazungumzo kati yao yaliangazia uimarishaji wa afya, upanuaji wa mpango wa nyumba za gharama nafuu, kufungua fursa za kibiashara na kuboresha mchango wa Wakenya wanaoishi ughaibuni kwa ustawi wa kitaifa.
Rais aliandamana na Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi na Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni miongoni mwa maafisa wengine wakuu serikalini. 
Share This Article