Watu 6 wafariki, zaidi ya 100 hawajulikani walipo mkasa wa feri Indonesia

Feri hiyo ilikuwa imebeba takriban watu 240 ilipopoteza mawasiliano huku jitihada za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya BBC

Watu 6 wamefariki huku wengine 130 wakiwa hawajulikani walipo baada ya feri kupoteza mawasiliano katika Bahari ya Java karibu na Indonesia. 

Feri hiyo ilikuwa imebeba takriban watu 240 wakati wa tukio hilo.

Mamlaka za utafutaji na uokoaji za nchi hiyo zimesema kampuni inayomiliki feri hiyo ilizifahamisha jana Jumapili asubuhi kwamba imepoteza mawasiliano na feri hiyo iliyokuwa  ikielekea Banjarmasin Kusini mwa Kalimantan.

Aidha, mamlaka zimesema operesheni ya utafutaji ilianzishwa mara moja na watu wapatao 100 kuokolewa.

Jitihada za utafutaji na uokoaji bado zinaendelea.

Feri hiyo iliondoka Surabaya Mashariki mwa Java Jumamosi wiki jana na kuripotiwa kukumbana na hali mbaya ya hewa.

Share This Article