Kindiki: Serikali inaimarisha ukuaji wa maendeleo na uchumi

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Kithure Kindiki.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, ameteta ajenda ya serikali ya Rais William Ruto, akidokeza kuwa inatekeleza miradi ya maendeleo na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Akizungumza wakati wa hafla ya uwezeshaji kiuchumi eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi, Kindiki alilaumu upande wa upinzani kwa kukosa ajenda ya taifa hili.

Alidokeza kuwa utawala wa Rais Ruto umejitolea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa usawa kote nchini kwa lengo la kubadilisha maisha ya wakenya.

“Sisi hufanya kazi Jumatatu hadi Jumatatu, Januari hadi Disemba. Hatuna wakai wa siasa zisizi na msingi ambazo huwapotosha wananchi,” alisema Kindiki.

Aliwahimiza wakenya kuzingatia maendeleo na ukuaji wa uchumi, akisema serikali ya sasa imechukua mkondo ufaao.

Website |  + posts
Share This Article