KCB watwaa taji ya kitaifa kwa mara ya tatu mtawalia

KCB walitawazwa mabingwa licha ya kushindwa katika nusu fainali ya msururu wa sita na wa mwisho wa Christie Sevens uliokamilika Jumapili katika uwanja wa RFUEA kaunti ya Nairobi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Kenya Commercial Bank imehifadhi taji ya kitaifa ya raga kwa wachezaji kumi na tano upande kwa kwa wanaume mara ya tatu mtawalia.

KCB walitawazwa mabingwa licha ya kushindwa katika nusu fainali ya msururu wa sita na wa mwisho wa Christie Sevens uliokamilika Jumapili katika uwanja wa RFUEA kaunti ya Nairobi.

Menengai Oilers wamenyakua ubingwa wa msururu wa Nairobi kufuatia ushindi wa alama 24-12, dhidi ya Strathmore Leos katika fainali.

Strathmore Leos waliwabandua KCB katika nusu fainali pointi 19-12, huku Menengai Oilers wakiwabwaga Kabras sugar 20-10.

KCB wametuzwa shilingi laki tatu kwa ubingwa huo huku Kabras wakipata laki moja unusu kwa kumaliza nafasi ya pili wakati Menengai wakituzwa laki moja katika baada ya kumaliza nafasi ya tatu.

Mwamba walinyakua taji ya wanawake ,wakifuatwa na Queens na Kiambaa Ladies katika nafasi za pili na tatu mtawalia.

Mashindano ya msururu wa kitaifa yalishirikisha mikondo ya;Dala Sevens katika kaunti ya Kisumu, Kabeberi Sevens ya Nairobi, Driftwood Sevens huko Mombasa na Embu kabla ya kumalizikia Nairobi kwa msururu wa Christie Sevens .

Share This Article