Ruto akutana na viongozi wa Kisumu,Siaya,Homa Bay na Migori

Kama njia ya kumuenzi kiongozi wa chama cha  ODM hayati marehemu Raila Odinga,  kwa kuimarisha ushirikiano baina ya chama hicho na  UDA kupitia kwa serikali jumuishi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amekutana na viongozi wa mashinani kutoka kaunti za Kisumu, Siaya, Homa Bay na Migori, huku akianza rasmi ziara ya siku nne katika eneo hilo la Nyanza.

Kwenye mkutano huo ulioandaliwa katika eneo la kutua kwa meli katika kaunti ya Kisumu ,Rais Ruto  alizungumzia agenda  za maendeleo ya eneo hilo na jinsi ya kuliinua kiamendeleo.

Kama njia ya kumuenzi kiongozi wa chama cha  ODM hayati marehemu Raila Odinga,  kwa kuimarisha ushirikiano baina ya chama hicho na  UDA kupitia kwa serikali jumuishi.

Rais alitaja ufanisi wa serikali yake katika kipindi cha miaka minne iliyopita ikiwemo kukwamua miradi ya maendeleo,na  kutimiza nyingi ya ahadi zake za kabla ya uchaguzi mkuu uliopita.

Awali Rais alihudhuria ibada katika kanisa la  Voice Of Salvation And Healing kaunti ya Kisumu.

Share This Article