Kijanangoma aahidi kufungua Kasri ya Ufalme wa Tooro kwa kila mmoja

Ufalme wa Tooro ni mojawapo wa Falme 5 za kitamaduni zinazaotambuliwa na serikali ya Uganda.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mfalme mteule wa Ufalme wa Tooro nchini Uganda,Edward Rukidi Kijanangoma ameahidi kuwa atafungua Ufalme huo kwa yeyeote atakayetaka kushauriana naye punde atakapoidhinishwa.

Kijanangoma ambaye ni Msomaji habari katika runinga ya shirika la utangazaji nchini Uganda (UBC) alipendekezwa kuwa mrithi wa Oyo Nyimba  Kabamba,aliyeazikwa Jumamosi baada ya kufariki akipokea matibabu nchini Marekani, kutokana na Saratani.

Kijanangoma alichaguliwa na jopo la wazee 21 kuwa Mfalme hatua ambayo imeibua mgawanyiko mkubwa huku familia ya marehemu Oyo Nyimba ikipinga vikali uteuzi huo.

Ufalme wa Tooro ni mojawapo wa Falme 5 za kitamaduni zinazaotambuliwa na serikali ya Uganda.

Share This Article