Gor Mahia kujaribu kupanda mchongoma Misri ,Jumapili usiku

Ni sharti Gor wapate ushindi sawia ili kusukuma mchuano kwa muda wa ziada.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara 22 wa Ligi Kuu ya Kenya,Gor Mahia FC, watakuwa na kibarua cha karne watakapomenyana na mabingwa wa Misri Pyramids FC,katika marudio ya mchujo wa kwanza kuwania taji ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchuano huo utapigwa katika uwanja wa June 30 jijini Cairo, huku wenyeji wakijivunia ushindi wa mabao 2-0, katika duru ya kwanza uwanjani Nyayo,Nairobi wiki jana.

Ni sharti Gor wapate ushindi sawia ili kusukuma mchuano kwa muda wa ziada.

Gor wanaofuzwa na Charles Akonor, walifanya mazoezi ya mwisho mapema Jumapili tayari kwa mechi hiyo ya Jumapili kuanzia saa mbili usiku.

Licha ya kushindwa nyumbani Nairobi,kocha Akonor ana imani ya kugeuza matokeo na kupata ushindi utakaowafuzisha kwa mchujo wa pili.

Share This Article