Ruto: Serikali imeimarisha uchumi wa taifa

Kulingana na Rais Ruto, alichukua hatamu za uongozi wakati ambapo uchumi wa Kenya ulikabiliwa na changamoto za gharama ya juu ya maisha.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto azindua ujenzi wa barabara katika kaunti ya Kericho.

Rais  William Ruto,  amesema serikali yake imeimarisha uchumi , kupunguza madeni , kudhibiti mfumuko wa bei  pamoja na kuboresha ubadilishanaji wa fedha za kigeni.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo leo Ijumaa kwenye ziara yake ya siku ya tatu katika eneo la South Rift.

Alisema uchumi wa Kenya umeimarika pakubwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na sasa uchumi wa taifa hili ni wa sita kwa ukubwa barani Afrika.

“Chini ya utawala wangu, madeni yameongezeka kwa asilimia 27 ikilinganishwa na ongezeko la mara tatu hadi tatu wakati wa serikali mbili za awali,” alisema Rais Ruto.

Kulingana na Rais Ruto, alichukua hatamu za uongozi wakati ambapo uchumi wa Kenya ulikabiliwa na changamoto za gharama ya juu ya maisha, viwango vya juu vya riba, deni kubwa, na matatizo ya fedha za kigeni.

Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa barabara ya kilomita 43 ya  Tegat-Kaplelit-Kokwet-Toroton eneo bunge  la Kipkelion Magharibi, kaunti ya Kericho.

Wakati huo huo, alizindua mradi wa uunganishaji umeme wa Last Mile wa kitita cha shilingi Milioni 420, katika eneo hilo.

Rais Ruto yuko kwenye ziara ya siku nne katika eneo la South Rift.

Share This Article