Pigo kwa IEBC, mahakama Kuu yasimamisha utoaji zabuni ya kuchapisha karatasi za kupiga kura

Jaji William Musyoka,alisimamisha utoaji zabuni kufuatia kesi iliyowalishwa na kampuni ya  Oilmax Ventures Limited Septemba 3 mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read
Erastus Ethekon - Mwenyekiti wa IEBC

Ni pigo kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC), baada ya Mahakama Kuu kusitisha mchakato wa utoaji zabuni ya uchapisahji karatasi na vifaa vya kupigia kura mwaka ujao.

Shughuli hiyo imesimamishwa baada ya mojawapo wa waliotuma maombi ya zabuni kuwasilisha keshi mahakamani kupiga masharti yaliyowekwa.

IEBC kwa sasa haina budi ila kusimamisha shughuli yote hadi pale kesi hiyo itakaposikizwa na kuamuliwa  kabla ya kutoa zabuni.

Jaji William Musyoka,alisimamisha utoaji zabuni kufuatia kesi iliyowalishwa na kampuni ya  Oilmax Ventures Limited Septemba 3 mwaka huu.

Kwenye kesi hiyo  Olimax inahoji baadhi ya masharti kama yale yanayotaka kampuni iwe impewa zabuni ya kusambaza angaa karatasi milioni 150, za kupigaji kura kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita hali anayosema inapendelea kampuni chache huku nyingi zikifungiwa nje.

Share This Article