Mamia ya raia wa Burundi walimiminika kwa siku ya tatu mfululizo katika ubalozi wa Nairobi, kusijasili ili kupata stakabadhi za kuishi na kufanya biashara nchini Kenya.
Haya yanajiri baada ya serikali kutoa makataa ya siku 90, kwa raia wote wa kigeni wanaoishi Kenya, kujisajili la sivyo watimuliwe.
Foleni refu zilishuhudiwa kwenye Ubalozi wa Burundi katikakati ya jiji kwa shughuli hiyo.
Kenya ina jumla ya wakimbizi 16,000 raia wa Burundi, wanaotafuta hifadhi ya ukumbizi huku idadi hiyo ikizidi kuongezeka kutokana na misukosuko ya kisiasa ambayo imekuwa ikishuhudiwa nchini mwao.
Wengi wa waliofika katika ubalozi wanahoji kuhofia maisha kufuatia agizo la Rai William Ruto wiki jana ,baadhi wakikiri kuhangaishwa na Wakenya .