Awendo Academy ya Migori na Sameta High School kutoka Kisii nio miongoni mwa timu 12 kutoka eneo la Nyanza zilizofuzu kwa mashindano ya Safaricom Chapa Dimba ,katika eneo la Nyanza baina ya Septemba 12 na 13.
Mashindano hayo yataandaliwa katika uwanja wa maonyesho ya kilimo wa Mamboleo.
Timu hizo 12 zilituzwa shilin 75,000, huku zilizomaliza nafasi za pili zikipokea shilingi 30,000.
Katika kaunti ya Kisumu Obunga FC waliibwaga Julu Nyambugu mabao 4-1 kupitia penati kufuatia sare tasa.
Mabingwa mara mbili wa kombe hilo Plateau Queens, zamani ikijulikana kama Nyakach Girls, walihifadhi taji ya wanawake kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Victoria Soccer Academy.
Katika kaunti ya Siaya, Indomitable Soldiers waliizaba Real Talent Academy 10-9, kupitia penati kufuatia sare ya bao moja na kushinda taji ya wavulana,nao Nyamira Starlets wakailemea Lwak Starlets penati 6-5, kutawazwa mabingwa kwa wasichana.
Huko Migori,Korwa walipigwa goli moja kwa sifuri na Awendo Academy, hukju Oyugi Ogango Girls, wakiipiku Mukuyu Queens 3-2 na kushinda taji ya wasichana.