Diamond na Zuchu watangaza tarehe ya sherehe ya siku 40 za mwanao

Sherehe hiyo itaandaliwa Septemba 12, 2026, huko Tegeta Madale kuanzia saa tisa alasiri.

Marion Bosire
1 Min Read

Wapenzi na nyota wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz na Zuchu, wanajiandaa kusherehekea hatua muhimu kwa mtoto wao wa kike, ambaye anatimiza siku 40 tangu kuzaliwa.

Kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii, wawili hao wametangaza tarehe ya sherehe hiyo maalum, ambayo ni Septemba 12, 2026, huku wakiendeleza mipango yao ya kumsherehekea mtoto huyo katika siku zake 40 za kwanza.

Tukio hilo litaandaliwa huko Tegeta Madale kuanzia saa tisa alasiri na linatarajiwa kuwakutanisha wanafamilia wa karibu, marafiki pamoja na baadhi ya nyota wenzao, kwa ajili ya kusherehekea ujio wa mwanachama huyo mpya wa familia.

Ijumaa Julai 31, 2026, Zuchu na Diamond waliandaa sherehe ya kumkaribisha mwanao ambaye hakuwa amezaliwa ambapo pia walifichua jinsia yake.

Zuchu alifanikiwa kupata salama Agosti 2, 2026 ambapo yeye na Diamond walichapisha picha akiwa kwenye chumba cha hospitali na bini yao.

Inasubiriwa kuona itakavyokuwa sherehe hiyo muhimu.

Share This Article