Rais William Ruto ameahidi kuinga timu za taifa za wanawake ,Harambee Starlets na Junior Starlets kwa hali na mali zinapojiandaa kwa mashindano ya kimataifa.
Rais amesema haya mapema Jumanne katika Ikulu ya Nairobi alipokabidhi bendera za taifa kwa timu hizo .
Aidha,Rais alikariri kujitolea kwa serikali yake kumarisha miundombinu ya michezo nchini ili kukuza vipaji.
Ruto alitoa changamoto kwa timu ya wanawake Harambee Starlets, kusajili matokeo bora inapoelekea fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON), nchini Morocco, kati ya Julai 26 na tarehe 16 mwezi ujao.
Pia Rais, alitia hamasa timu ya chipukizi ya Junior Starlets, ambayo imefuzu kwa Kombe la Dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17,kwa mara ya pili.

Starlets ambayo imefuzu kwa kombe la WAFCON, kwa mara ya pili tangu mwaka 2016, itafungua kampeni yake nchini Morocco tarehe 26 mwezi huu, dhidi ya wenyeji kundini A,kabla ya kuchuana na Algeria na Senegal.
Timu nne bora katika mashindano hayo zitafuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil.
Upande wake Junior Starlets ilifuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili mwaka huu baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2024.

Vipusawa Junior Starlets wanaofunzwa na kocha Mildred Cheche, wamejumuishwa kundi E, pamoja na Samoa,China na Marekani, huku kipute hichi kikiandaliwa kati ya Oktoba 17 na Novemba 7, mwaka huu nchini morocco.