Rais wa soka nchini Saudi Arabia Yasser Al-Misehal, ajiuzulu

Saudi Arabia ilibanduliwa Kombe la Dunia kwa pointi mbili baada ya kutoka sare na Cape Verde na Uruguay na kushindwa magoli 4-0 na Uhispania.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Shirikisho la soka nchini Saudi Arabia (SAFF) Yasser Al-Misehal, amejiuzulu leo Jumatatu, kufuatia kubanduliwa kwa timu yao kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Kung’atuka kwa Yasser kunakamilisha muhula wa miaka saba akiwa katika uongozi wa SAFF .

Kupitia kwa ukurasa wa X, Yasser amesema anachukua jukumu la matokeo mabaya ya timu ya taifa iliyobanduliwa kutoka  Kombe la Dunia, katika hatua ya makundi.

Saudi Arabia ilibanduliwa Kombe la Dunia kwa pointi mbili baada ya kutoka sare na Cape Verde na Uruguay, na kushindwa magoli 4-0 na Uhispania.

Saudi imeshiriki Kombe la Dunia mara saba na imefuzu mara moja pekee kwa mechi za mwondoano iliposhiriki mara ya kwanza mwaka 1994.

Shirikisho la SAFF lilielekezewa kidole cha lawama kwa matokeo hayo duni, wengi wakihoji mipangilio iliyopo ya ukuzaji talanta,uteuzi wa wachezaji na maamuzi duni ya kiufundi.

Share This Article