Tarehe mpya ya kipute cha CHAN yatangazwa na CAF

CAF iliahirisha mashindano hayo kutoka Februari hadi Agosti ili kutoa fursa kwa mataifa hayo matatu kujiandaa vyema.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF, limetangaza tarehe mpya ya kuandaliwa kwa makala ya nane ya fainali za kombe la Afrika kwa wachezaji wa nyumbani, CHAN.

Kulingana na taarifa ya CAF, baraza kuu lililokutana jijini Rabat, Morocco, Januari 27, fainali hizo zitakazoandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda, na Tanzania zitafanyika kati ya Agosti 2 na 30.

CAF iliahirisha mashindano hayo kutoka Februari hadi Agosti ili kutoa fursa kwa mataifa hayo matatu kujiandaa vyema.

Kulingana na droo iliyoandaliwa tarehe 15 mwezi huu jijini Nairobi, wenyeji Kenya wamejumuishwa kundi A pamoja na mabingwa mara mbili, Jamhuri ya Kidemokratia ya Congo na Morocco, pamoja na Zambia.

Waandalizi wenza Tanzania wamo kundini B pamoja na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kundi C linajumuisha waandalizi wenza Uganda, Niger, Guinea, na timu mbili zitakazofuzu huku mabingwa watetezi Senegal wakiwa kundi D pamoja na Congo Brazzaville, Sudan, na Nigeria.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article