Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi akamatwa kwa madai ya ufisadi

Uchunguzi ulibainisha kuwa cheti cha ushuru kilichowasilishwa wakati wa utoaji kandarasi hiyo, kilikuwa bandia na hakikutolewa na Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru Nchini (KRA).

Tom Mathinji
1 Min Read
Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi akamatwa kwa madai ya ufisadi.

Maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi EACC,  wamemkamata Mkurugenzi wa kampuni moja ya Ulinzi anayehusishwa na ulaghai  katika utoaji wa  kandarasi  ya shilingi milioni 5.4 katika Taasisi ya Kiufundi ya Keroka.

Mshukiwa huyo Gilbert Momanyi Maturwe, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi na uchunguzi ya  Gimo, alitiwa nguvuni baada ya kukamilika kwa uchunguzi kuhusu utoaji kandarasi hiyo, baada ya kubainika kuwa  kampuni hiyo ilipata kandarasi ya shilingi 257,000 kwa mwezi, kwa kipindi cha miaka miwili ambazo ni jumla ya shilingi 5,448,000.

Hata hivyo, licha ya kupungua kwa idadi ya walinzi wanaotumwa na kampuni hiyo, malipo hayo yaliendelea kutolewa kwa kiwango cha awali.

Uchunguzi huo pia ulibainisha kuwa cheti cha ushuru kilichowasilishwa wakati wa utoaji kandarasi hiyo, kilikuwa bandia na hakikutolewa na Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru Nchini (KRA).

EACC iliwasilisha ripoti ya uchunguzi wake kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, aliyeidhisha mashtaka hayo.

Mshukiwa huyo alifikishwa kwenyw Mahakamani  ya Hakimu Mkuu wa Kisii, ambako alikanusha mashtaka dhidi yae na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moka.

TAGGED:
Share This Article