Mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Iran kuanza tena wiki ijayo

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kwa sasa yupo ziarani Mashariki ya Kati

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ameashiria kuwa mazungumzo ya kiwango cha kitaalam kati ya nchi hiyo na Iran yanaweza kuanza tena juma lijalo.

Akiwahutubia wanahabari nchini Kuwait jana Jumatano, Rubio alisema watu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ile ya Nishati watashiriki mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika nchini Uswizi.

Iran imeonekana kupinga wakaguzi wa nyuklia kuingia nchini humo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Kazem Gharibabadi ameashiria kuwa hakuna mipango ya kuruhusu ukaguzi wa nyenzo za nyuklia au maeneo yaliyoharibiwa.

Ameongeza kuwa Marekani lazima iondoe vikwazo ilivyowekea nchi hiyo kwanza kabla ya hilo kuwaziwa.

Share This Article