Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola awasili Kenya kwa ziara rasmi

Botchwey, anatarajiwa kushiriki mazungumzo na viongozi wa serikali na wadau wengine muhimu.

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Shirley Ayorkor Botchwey, awasili Kenya kwa ziara rasmi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Shirley Ayorkor Botchwey, amewasili Kenya kwa ziara rasmi.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo.

Botchwey, anatarajiwa kushiriki mazungumzo na viongozi wa serikali na wadau wengine muhimu kuhusu uongozi, maendeleo endelevu, kuwawezesha vijana, biashara, usalama na amani katika kanda hii.

Ziara hiyo inajiri wakati ambapo Kenya inaendelea kutekeleza majukumu muhimu katika maswala ya Jumuiya ya Madola, huku mazungumzo yakilenga kuboresha ushirikiano ili kufanikisha ukuaji, demokrasia katika uongozi na udhabiti wa kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama.

Mazungumzo hayo pia yatatoa fursa nzuri wa kuangazia maswaka yanayowaathiri raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

TAGGED:
Share This Article