Maafisa wa polisi waagizwa kukabiliana na magenge ya wahalifu

Kanja aliwaonya maafisa wa polisi dhidi ya kuzembea kazini huku akithibitisha kujitolea kwa Huduma ya Taifa ya Polisi kulinda maisha na mali ya Wakenya.

Tom Mathinji
1 Min Read
Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas kanja.

Maafisa wa polisi wameagizwa kubabiliana na ongezeko la magenge ya wahalifu yanayowakosesha usingizi wananchi kote nchini.

Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja ameonya dhidi ya kuibuka tena kwa makundi hayo ya wahalifu, akisisitiza umuhimu wa kuwa na uwajibikaji katika huduma ya polisi.

Akiwahtubia Maafisa Wakuu wa Polisi katika taasisi ya mafunzo ya polisi huko Ngong, Kanja aliwataka maafisa hao kubuni mikakati kabambe kuhakikisha uzingatiaji sheria na utulivu kwa Wakenya, wakazi na wageni wanaozuru taifa hili.

Kwenye mkutano huo, Kanja aliwaonya maafisa wa polisi dhidi ya kuzembea kazini, huku akithibitisha kujitolea kwa Huduma ya Taifa ya Polisi kulinda maisha na mali ya Wakenya.

Wakati huo huo, aliwapongeza maafisa wa polisi kwa juhudi zao za kukabiliana na uhalifu na hatari zingine za kiusalama katika pembe zote za Kenya.

Katika mkutano huo, Kanja aliandamana na Manaibu Inspekta Mkuu wa Polisi Eliud Lagat na Gilbert Masengeli, na Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Mohamed Amin.

Share This Article