Waandalizi wenza wa patashika ya Kombe la Dunia mwaka huu Canada walilazimishwa kutoka sare ya bao moja na Bosnia Herzegovina,katika mchuano wa ufunguzi wa kundi D Ijumaa usiku uwanjani BMO mjini Toronto.
Wageni Bosnia walichukua uongozi kunako dakika 24 kupitia kwa Sead Kolasinac, alipounganisha mkwaju wa kona yake Ivan Basic na kuongoza hadi mapumziko.
Wenyeji the Reds walirejea kipindi cha pili mataio ya juu wakimiliki mpira na kupiga mashambulizi ya kujibu mara kwa mara.
Hata hivyo,Bosnia ukipenda ‘The Dragons’walijihami kwa muda mrefu wa kipindi cha pili.
Nguvu mpya wawili wa Cananada Cyle Larin na Promise David, walishirikiana vyema huku Promise, akivurumiza tobwe kusawazisha dakika 12 kabla ya kipenga cha mwisho.
Ilikuwa pointi ya kwanza kwa Canada ,wakishiriki Kombe la Dunia kwa mara ya tano.