Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC)imeidhinisha matumizi ya mtandao wa Internet wa Star Link.
Hafla hiyo iliandaliwa Ijumaa na kushuhudiwa na Rais Yoweri Museveni.
Awali Januari mwaka huu Museveni, alifunga matumizi ya Star Link wakati wa uchaguzi mkuu kwa kutofuata sheria za usajili ipasavyo.
Akizungumza Ijumaa ,Museven,i alisema matumizi ya Star Link nchini humo yataongeza upatakinaji na usalama wa huduma za Internet.
Star Link inatarajiwa kuongeza kiwango cha Internet nchini Uganda kwa zaidi ya asilimia 50,hususan katika maeneo ya mashinani.
Pia kampuni ya Star Link inatarajiwa kubuni fursa za ajira na kutoa ushindani kwa kampuni ya mawasiliano ya MTGN inayotoa huduma za Internet kwa kiwango cha juu nchini Uganda.