Kenya yatia saini Mikataba ya Maelewano na Finland

Mikataba hiyo ya kiuchumi ni pamoja na Mabadiliko ya Tabianchi,Elimu, Digitali na Uvumbuzi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya yatia saini Mikataba ya Maelewano na Finland.

Kenya na Finland zimetia saini Mikataba ya Maelewano katika hatua ya kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili.

Rais William Ruto alisema mikataba hiyo ya kiuchumi ni pamoja na Mabadiliko ya Tabianchi,Elimu, Digitali na Uvumbuzi.

Kiongozi wa taifa ambaye yuko kwenye ziara rasmi ya kiserikali nchini Finland, alisema kimataba hiyo pia itafanikisha ushirikiano wa kisayansi, ubadilishanaji wa maarifa na kuimarisha  uvumbuzi unaochochea maendeleo endelevu na ustawi wa pamoja wa raia wa nchi hizo mbili.

Kwenye hafla hiyo, Rais Ruto alisema Kenya na Finland zilikubaliana kuimarisha taasisi za mataifa hayo ili ziboreshe uwakilishi na uwezo wa kukabiliana na changamoto ibuka.

“Fauka ya hayo tulielezea kujitolea kwetu kufanikisha upatikanaji wa amani, kuheshimu maadili ya mataifa yote na utatuzi wa mizozo kuambatana na sheria za kimataifa,” alisema Rais Ruto.

Rais wa Finland Alexander Stubb alishuhudia hafla hiyo iliyoandaliwa katika Ikulu ya Rais Jijini Helsinki.

Share This Article