Rais Ruto: Serikali kufadhili elimu ya juu kikamilifu

Ruto alisema taifa hili linapaswa kuwekeza kwa elimu kwa sababu inampa kila mwanafuzni aliyefuzu fursa sawa ya ufanisi bila kujali familia alikotoka.

Tom Mathinji
2 Min Read
Rais William Ruto.

Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu na vyuo anuwai sasa wana kila sababu ya kutabasamu, baada ya serikali kusema itawafadhili kikamilifu kupitia mfumo mpya uliopendekezwa na Rais William Ruto.

Akizungumza leo Jumanne katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alisema hatua hiyo itahakikisha kila mwanafunzi anayejiunga na elimu ya juu anapata fursa ya kuendelezsa masomo yake bila kukabiliwa na changamoto za kifedha.

Ametoa wito kwa Bunge la Taifa kupitisha sheria iliyofanyia marekebisho Bodi ya Kutoa Mikopo kufadhili Elimu ya Juu (HELB), ili mfumo huo mpya wa ufadhili utumike kwa wanafunzi wanaojiunga na taasisi hizo mwezi Septemba mwaka 2026.

”Kuanzia sasa, kila mwanafunzi ambaye amefuzu kujiunga na vyuo anuwai au vyuo vikuu, atafadhiliwa kikamilifu. Lakini wazazi watakuwa na uhuru wa kulipa karo iwapo wanataka,” alisema Rais Ruto.

Alisema taifa hili linapaswa kuwekeza kwa elimu kwa sababu inampa kila mwanafuzni aliyefuzu fursa sawa ya ufanisi bila kujali familia alikotoka.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo alipokuwa akipokea ripoti kuhusu Ruwaza Mpya ya Taifa inafafanua Mikakati ya muda mrefu ya mageuzi ya nchi hii kwenye hafla iliyoandaliwa katika Ikulu ya Nairobi.

Alisema ripoti hiyo inaleta mchango mkubwa kwa mjadala muhimu wa kitaifa, huku ukipanua mawazo yetu kuhusu maamuzi ambayo yatabadilisha mustakabali wa taifa hili.

“Nafurahia kwamba maswala mengi yaliyoangaziwa kwenye ripoti hii, yanazunguzia mwelekeo wa kimkakati ambayo ytayari tumeanza kutekeleza,” alisema Rais Ruto.

TAGGED:
Share This Article