Shirika la Posta nchini Kenya litafunga matawi yake 125, kufikia mwisho wa mwezi ujao kama njia ya kupunguza gaharama.
Posta iliyopo na matwi 625 kote nchini huku hatua hiyo kitarajiwa kupunguza gharama yake kwa asimili 20.
Shirika la Posta limekuwa katika hali ngumu huku wafanyakazi wakienda kwa miezi kadhaa bila malipo.
Tayri matawi kadhaa yamefungwa huku Posta, ikilenga kusalia na matawi 500 kote nchini.
Aidha, wafanyakazi walioathiriwa kwa kusimamishwa kazi tayari wamejuzwa.