Waziri Kagwe aapa kukomesha uchuuzi wa maziwa

Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe amesema wamenasa mitambo 25 ya kuhifadhi maziwa katika eneo la Uhuru Park, jijini Nairobi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imeanzisha msako kote nchini Kenya kwa lengo la kukabialiana na wachuuzi wa maziwa ambayo hayajaidhinishwa.

Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe amesema wamenasa mitambo 25 ya kuhifadhi maziwa katika eneo la Uhuru Park, jijini Nairobi.

Kagwe ameongeza kuwa maziwa hayo ni hatari kwa usalama na afya ya wanaoyatumia kwani hayajaidhinishwa, akiapa kumaliza biashara hiyo haramu.

“Uchuuzi wa maziwa ni sharti ukomeshwe. Ni hatari kwa afya na unamaliza uwezo wa kuongeza thamani,” amesema Kagwe.

Ameongeza kuwa mageuzi kadhaa katika sekta ya maziwa yanafanywa ili kuhakikisha Kenya inauza maziwa ya thamani na yenye ubora nje ya nchi.

Share This Article