FIFA World Cup 2026:Siku 30 kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia

Jumla ya timu 48 zitashiriki na mechi 104 kutachezwa katika viwanja 16 tofauti huku fainali ikipigwa Julai 19.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ikiwa Jumanne Mei 12 mwaka 2026,zimesalia siku 30 pekee, kabla ya kung’oa nanga kwa makala ya 23, ya kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia kitakachoandaliwa kwa pamoja na Marekani,Canada na Mexico.

Jumla ya timu 48 zitashiriki na mechi 104 kutachezwa katika viwanja 16 tofauti huku fainali ikipigwa Julai 19.

Kati ya miji 16 itakayoandaa fainali hizo 11 ni ya Marekani.

Miji ya Marekani ni pamoja na Dallas,Atlanta,Boston,Houston,Kansas,Los Angeles,Miami,New York,Philadelphia,San Francisco na Seattle.

Miji ya Canada ya Kombe la Dunia ni pamoja na Toronto na Vancouver, wakati Mexico ikiwa Mexico City,Guadarajala na Monterray.

Itakuwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kuwa na mataifa 48 yakiwemo 10 ya Afrika.

Share This Article