Motsepe apongeza Kenya,Tanzania na Uganda kwa matayarisho ya AFCON 2027

Motsepe aliandamana na kaimu Katibu Mkuu Samson Adamu,Rais wa TFF Wallace Kaaria na Kinara wa FUFA Moses Magogo, pamoja na maafisa wa serikali husika.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe, amepongeza hatua zilizopigwa na Kenya,Uganda na Tanzania, kwa matayarisho ya fainali za kombe la AFCON mwaka ujao.

Motsepe amesema haya Jumatatu alipokutana na viongozi wa serikali na mashirikisho ya soka hayo matatu jijini Nairobi pembezoni mwa kongamano la Africa Forward .

Kenya,Uganda na Tanzanoa zitaandaa makala ya 36 ya kipute cha AFCON baina ya Juni na Julai mwaka ujao.

Motsepe aliandamana na kaimu Katibu Mkuu Samson Adamu,Rais wa TFF Wallace Kaaria na Kinara wa FUFA Moses Magogo, pamoja na maafisa wa serikali husika.

Share This Article