Rais Ruto wajadiliana na Rais wa Gabon, Brice Oligui Nguema

Mataifa hayo mawili yalikariri kujitolea kuhubiri na kuimarisha amani na kuwalinda raia wao na kupiga jeki maendeleo endelevu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumatatu amefanya mazungumzo na mwenzake wa Gabon, Brice Oligui Nguema,katika Ikulu ya Nairobi.

Nguema yuko nchini kwa ziara rasmi kuhudhuria kongamano la Africa Forward Summit.

Viongozi hao wawili waliafikiana kuimarisha ushirikiano katika wizara ya elimu kupitia kwa msaada wa masomo ,elimu ya kiufundi na mipango ya kubadilishana ujuzi.

Mataifa hayo mawili yalikariri kujitolea kuhubiri na kuimarisha amani na kuwalinda raia wao na kupiga jeki maendeleo endelevu.

Kenya na Gabon, waliafikiana kuwa katika mstari wa mbele kueneza amani barani afrika na kutafuta suluhu ya kudumu kwa mizozo ya maziwa makuu na upembe wa Afrika.

Aidha,Rais Ruto alichukua fursa hiyo kmpigia debe Jaji wa Mahakama ya upeo Njoki Ndung’u, anayewania kuchaguliwa kuwa Jaji katika Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC.

Share This Article