Inter Milan walinyakua ubingwa wa 21 wa Ligi Kuu nchini Italia,Serie A, maarufu kama Scudetto kufuatia ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Parma, ugani San Siro Jumapili usiku.
Inter wanaofunzwa na Cristian Chivu,walihitaji tu alama moja ili watawazwe mabingwa baada ya wapinzani wa karibu Napoli, kutoka sare tasa na Como, siku ya Jumamosi.
Ulikuwa ushindi wa tano mtawalia kati ya mechi sita za nyumbani kwa Inter, ambao sasa wamecheza mechi 11 bila kushindwa.
Taji hiyo ni pili ya Scudetto kwa Inter Milan ndani ya kipindi cha miaka mitatu.