Harakati za Gor Mahia kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Kenya kwa mara ya 22, zilipigwa jeki baada ya kuwashinda Kakamega Homeboyz, bao moja kwa bila katika mechi ya raundi ya 30, iliyosakatwa Jumapili uwanjani Mumias Complex.
K’ogalo waliocheza mechi 30,wametanua uopngozi wao kileleni pa jedwali kwa pointi 9, zaidi ya wapinzani wa karibu AFC Leopards, walio na mchuano mmoja mkobani.
Police FC wanashikilia nafasi ya tatu kwa alama you 48, moja zaidi ya Homeboyz na Shabana, walio katika nafasi za nne na tano mtawalia.
Sofapaka iliyopandishwa ngazi mwaka 2009, na kutwaa taji hiyo hatimaye imeshushwa ngazi ikiburura mkia kwa pointi 18.
Nafasi mbili za mwisho kushuka ngazi ni kivumbi baina ya timu tano ;Bidco United iliyo ya 17 kwa alama 24,Kariobangi Sharks iliyo ya 16 kwa alama 30,Ulinzi Stars na APS Bomet zenye alama 31, kila moja na Posta Rangers iliyo na alama 32.
Gor walitawazwa mabingwa kwa mara ya mwisho msimu wa mwaka 2023-2024.