Elysee Bigira mwimbaji wa nyimbo za injili nchini rwanda, ametoa wimbo wa kuabudu alioupa jina la “Mutima Wanjye” wa urefu wa dakika 28.
Kazi hiyo ilikuwa sehemu ya juhudi za Elysee za kuandaa wapenzi wa nyimbo za injili kwa awamu ya pili ya tamasha yake kwa jina “Gifted For His Glory” aliyoandaa jana Jumamosi Mei 9, huko Brussels, Ubelgiji.
Wimbo huo ulioandikwa na Alaram Ministries unamweka yeyote anayesikiliza katika hali ya kufanya ibada na kujitoa kabisa kwa Mungu, ujumbe uliopo ukiangazia kujitolea, shukrani na imani maishani.
Bigira alielezea kwamba wimbo huo umejikita katika misingi ya kutoa moyo kabisa kwa Mungu, kuabudu na kumtukuza katika kila mapito ya maisha.
Tamasha ya Elysee ya Brussels iliangaziwa sana kutokana na uwepo wa waimbaji wa nyimbo za injili ambao ni wanandoa kutoka Rwanda Ben na Chance.
Siku chache kabla ya tamasha hiyo, Elysee na Ben & Chance walitangaza kwamba asilimia 80 ya tiketi za tamasha hizo zilikuwa zimenunuliwa tayari, ishara ya msisimko uliokuwepo kati ya wapenda nyimbo za injili.
Kabla ya tamasha yake ya Brussels, Elysee alidhihirisha imani ya mazuri akisema walikaribishwa vyema na aliamini kwamba tamasha hiyo ingekuwa na mvuto sawa na ile aliyoandaa katika BK Arena, nchini rwanda.
Kuhusu urafiki wa karibu na Ben & Chance, Elysee alifichua kwamba amefahamu wawili hao kwa miaka mingi, hata kabla yao kufunga ndoa.