Babake msanii maarufu wa muziki ulimwenguni Rihanna aiywate Ronald Fenty amefariki akiwa na umri wa miaka 70.
Mzee huyo anaripotiwa kufariki jana Jumamosi asubuhi huko Los Angeles Marekani kulingana na kituo kimoja cha redio cha Barbados alikozaliwa Rihanna.
Kituo hicho cha redio cha Starcom Network kilielezea pia kwamba mzee huyo alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi na kwamba watu wa familia yake wamekusanyika California kumuenzi.
Sio mengi yanafahamika kuhusu kuugua kwa mzee Fenty lakini Jumatano mwanawe aitwaye Rajad Fenty alionekana akifika kwa gari lake katika hospitali ya Cedars-Sinai iliyoko Los Angeles kumjulia hali. Rihanna naye akiaminika kuwa kwenye gari hilo.