Kenya yakosa medali mbio za Dunia kupokezana kijiti

Dismas Otuke
1 Min Read

Kinyume na mwaka jana iliponyakua shaba,timu ya Kenya imeambulia patupu katika mbio za Dunia za kupokezana kijiti zilizokamilika Jumapili nchini Botswana.

Timu ya mita 400 kwa wanariadha wanne mseto ilimaliza ya nne kwenye fainali ya Jumapili, nyuma ya Jamaica,Marekani na Uingereza zilizoshinda dhahabu,fedha na shaba mtawalia.

George Mutinda alianza vyema akitimka mzunguko wa kwanza kwa sekunde 45.31,akifuatwa na Mercy Chebet, aliyekimbia sekunde 51.04 ,nayek Kevin Kiprotich, akakamilisha mzunguko wake kwa sekunde 44.12, kisha Mercy Oketch, akakamlisha kwa sekunde 49.46.

Kenya iliwakilishwa na timu tano huku nne zikikosa kufika fainali.

Jamaica na Marekani wametawala mashindano hayo wakinyakua dhahabu 2 kila moja huku wenyeji Botswana na Norway, wakishinda dhahabu moja kila moja.

Jamaica imeshinda dhahabu ya mita 100 kwa wanariadha wanne mseto na mita 100 kwa wanawake .

Marekani iliwika katika mita 100 kwa wanaume na mita 400, huku Norway ikidedea katika mita 400 kwa wanawake nao wenyeji Botswana, wakatamba katika mita 400 wanaume wakiongozwa na Letsile Tebogo.

Share This Article