Serikali imebaini maeneo 59 yanayokabiliwa na hatari ya kukumbwa na mafuriko katika kaunti ndogo tano za kaunti ya Tana River na maeneo mengine nchini Kenya.
Maeneo 32 katika kaunti ndogo ya Tana Delta, yamo hatarini kwa mafuriko huku mengine 10 yakiwa katika kaunti ndogo ya Tana River, na mengine manane katika kaunti ndogo ya Bangale.
Sehemu nyingine zenye hatari ya mafuriko ni Nairobi,Rift Valley,Pwani,Central Kenya na Mashariki.
Maeneo hayo yamebainishwa kufuatia kuongezeka kwa viwango vya maji katika mabwawa ya Seven Folks.
Kaunti ya Nairobi imeripoti watu 6,600 waliohama makwao kutokana na mafuriko.
Tayari watu 18 wameripotiwa kuaga dunia kutokana mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini.
Serikali imewataka Wakenya kuchukua tahadhari wakati huu wa mvua nyongi kote nchini.