Mama Taifa Rachel Ruto ameongoza juhudi za ukarabati wa shule ya msingi ya Unoa kaunti ya Makueni, hii ikiwa hatua kubwa katika kuboresha mazingira ya msomo kwa wanafunzi na jamii inayopakana na shule hiyo.
Juhudi hizo ni pamoja na kuchimbwa kwa kisima,kuwekwa kwa matangi ya kuhifadhi maji pamoja na uzinduzi wa mradi wa umeme unaotokana na miyale ya jua kwenye shule hiyo.
Mama wa taifa alizuru shule hiyo mara ya kwanza mwaka jana ambapo alijionea hali ngumu ya masomo iliyokuwa ikiwakumba wanafunzi.
Mama Taifa alifurahia marekebisho yaliotekelezwa kwenye shule hiyo huku akikariri kuwa serikali chini ya uongozi wa rais William Ruto,itaendele kuwekeza kwa wanafunzi kupitia ujenzi wa mindomsingi bora, masomo kupitia mfumo wa dijitali na utoaji wa huduma za maji kwa shule.
“Uwanja uliokuwa na vumbi sasa umekarabatiwa na kuwa mazingira bora kwa masomo, madarasa yaliyokarabatiwa na shamba la shule ambalo linawakuza wanafunzi kimasomo na lishe bora,” alisema Mama Rachel.
Mama wa taifa pia alitoa wito wa ushirikiano wa karibu kati ya jamii na serikali katika kuzindua mazingira bora ya masomo kwa wanafunzi.