Sherehe za Sikukuu ya Mashujaa 2026 zitaandaliwa katika kaunti tatu za Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet na Nandi.
Hayo yalibainika leo Alhamisi wakati wa mkutano wa Kamati Simamizi ya Sherehe za Kitaifa uliofanyika chini ya uongozi wa Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen kuangazia maandalizi ya sherehe hizo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Katibu Dkt. Raymond Omollo na Magavana Jonathan Bii wa Uasin Gishu na Wisley Rotich wa Elgeyo Marakwet miongoni mwa wengine.
Kamati hiyo ikidokeza kuwa shamrashamra za kuadhimisha sikukuu hiyo zitakazoandaliwa wiki moja kabla ya sherehe kuu zifanyika katika miji ya Eldoret, Iten na Kapsabet chini ya kaulimbiu ya “Usalama na Michezo”.

Sherehe za Sikukuu ya Mashujaa huandaliwa Oktoba 20 kila mwaka kuwaenzi watu ambao wametoa mchango mkubwa kwa ujenzi wa taifa.