Joseph Kabila awekewa vikwazo na Marekani

Tom Mathinji
1 Min Read
Aliyekuwa Rais wa DRC Joseph Kabila.

Marekani imemwekea vikwazo aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa tuhuma za kuunga mkono waasi wa kundi la M23 na kusababisha ghasia za kisiasa  Mashariki mwa nchi hiyo.

Kulingana na Marekani, kundi la M23 na washirika wake wa Congo River Alliance (AFC), limekuwa likisababisha machafuko Mashariki mwa DRC, na kusababisha maafa na maelfu ya raia huku wengine wengi wakiachwa bila makao.

Aidha, Kabila anadaiwa kufadhili shughuli za kundi la ​AFC, ili kutoa ushawishi wa kisiasa Mashariki mwa DRC, akiwahimiza wanajeshi wa DRC kuasi na kujiunga na wapiganaji wa AFC.

Wakati huo huo, Kabila anadaiwa kujizatiti kupata umaarufu wa kisiasa dhidi ya serikali, kwa kumuunga mkono mpinazani wa kiongozi wa taifa hilo.

Chini ya uamuzi huo, mali zote za Kabila nchini Marekani zimezuiwa.

Naibu Waziri Mkuu wa DRC Jacquemain Shabani, alikaribisha hatua hiyo ya Marekani, akisema ilipaswa kutekelezwa kitambo.

“Yeye ni mchochezi, na chanzo cha ukosefu wa udhabiti nchini Congo. Kabila ni miongoni mwa wale wanaohujumu juhudi za kuleta amani nchini DRC,” alisema Shabani.

Share This Article