Uganda yaanza kutoa chanzo ya virusi vya UKIMWI

Dismas Otuke
1 Min Read

Uganda imeanza zoezi la kitaifa la kutoa chanjo dhidi ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI ijulikanayo kama Lanacapavir .

Akizungumza siku ya Ijumaa wakati wa kuzindua utoaji wa chanjo hiyo kwa ushirikiano na shirika la Global Fund  na serikali ya Marekani,Waziri wa Afya nchini Uganda  Dkt.Jane Ruth Aceng, aliwatahadharisha wananchi dhidi ya mienendo mibaya  ambayo huchangia maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Alionya kuwa ingawa chanjo hiyo inazuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa miezi sita, kamwe haizuii kuambukizwa magonjwa ya zinaa.

Uganda ni mojawapo wa mataifa yenye viwango vya juu vya maambukizi ikinakili visa vipya 37,000 mwaka jana huku wengine zaidi ya milioni 1.4, wakitumia dawa za kuzuia makali ya UKIMWI maarufu kama ARVs.

Chanjo hiyo hutolewa mara mbili kwa mwaka na Uganda inalenga kufikia vituo 300 vya umma vitakakavyotoa huduma hiyo ifikiapo mwishoni mwa mwaka huu.

 

Share This Article