Polisi wanasa mihadarati katika mpaka wa Kenya na Uganda

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa wa Polisi kutoka kaunti ndogo ya Teso Kaskazini, kaunti ya Busia, Magharibi mwa Kenya, wamenasa mihadarati wakati wa doria ya kawaida kwenye barabara yà Malaba – Uganda.

Maafisa hao waliokuwa wakipiga doria walikutana na mtu aliyekuwa na mifuko miwili karibu na kituo cha mabasi. Alipowaona maafisa hao, aliacha mifuko hiyo na kutoroka.

Baada ya kupekua mifuko hiyo, maafisa hao walipata vipande kadhaa vya bangi, vilivyopekekwa katika kituo cha polisi cha Malaba.

Kupitia ukurasa wa X, polisi walisema msako dhidi ya mshukiwa huyo umeanza

“Doria za kiusalama katika eneo hili zinaendelea ili kuimarisha juhudi za kukabiliana na uhalifu wa mpakani,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi.

Huduma hiyo ilitoa wito kwa wananchi kutoa habari kuhusu shughuli zinazotiliwa shaka kwa maafisa wa polisi kupitia nambari za dharura  999 au 911.

TAGGED:
Share This Article