Mabanati wa Kenya kumaliza udhia na Uganda kesho

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 17, imeratibiwa kuchuana na Uganda kesho jioni ugani Ulinzi Sports Complex katika marudio ya raundi ya pili kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Junior Starlets ya Kenya inajivunia uongozi wa mabao 2-0 kutoka na mkumbo wa kwanza wiki jana jijini Kampala, Uganda.

Mshindi wa pambano hilo atafuzu kwa raundi ya tatu atakapochuana na Cameroon.

Kenya wanalenga kufuzu kwa Kombe la dunia baadaye mwaka huu nchini Morocco, kwa mara ya pili baada ya kufuzu kwa fainali za mwaka jana katika Jamhuri ya Dominika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *