Mwigizaji maarufu wa filamu kutoka Hollywood, Omari Hardwick, amewasili Kenya kwa ziara rasmi.
Hardwick, ambaye ni maarufu kwa sinema ijulikanayo Power, amewasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, mapema leo ambapo anatarajiwa kuhudhuria hafla kadhaa ikiwemo kufungua jumba la HQ Kenya House katika eneo la Tatu City.
Akizungumza alipowasili JKIA, Harwick amesema, “Nalenga kueneza biashara yangu humu nchini na pia kutathmini fursa zilizopo kibiashara kwa kutumia jina langu.”
HQ Kenya House ni jumba la burudani ambalo ni sawia na lile la HQ DC House mjini Washington DC, nchini Marekani, na linamilikiwa na Burns Brothers, Mike na John.
Jumba hilo hujumuisha burudani, utamadani, jamii, na kuwa na vinyago ili kuwafurahisha wateja.
Akiwa nchini Omari anatarajiwa kukutana na wasanii kadhaa wa humu nchini.