Mswada wa Fedha 2024: Mjadala waanza bungeni

Martin Mwanje
1 Min Read

Wabunge katika bunge la taifa wameanza kujadili Mswada wa Fedha 2024 ambao katika siku za hivi karibuni umezua cheche za kisiasa nchini.

Hatima ya mswada huo itajulikana baada ya wabunge kuujadili baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza na pili na kisha kuupigia kura yamkini baadaye wiki ijayo.

Katika mjadala ulioanza leo Jumatano, wabunge walionekana kuunga mkono ama kupinga mswada huo kulingana na mirengo yao ya kisiasa.

Wabunge wa Azimio wameapa kupinga mswada huo wakati wa kuupigia kura bungeni.

Hata hivyo, wenzao wa Kenya Kwanza wameapa kuunga mkono mswada huo wakisema mapendekezo tata ya utozaji ushuru yataondolewa kama ilivyopendekezwa na kamati ya fedha ya bunge.

Mwenyekiti wa kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Molo Kuria Kimani jana Jumanne ilitangaza kutupiliwa mbali kwa mapendekezo kadhaa tata kutoka kwa Mswada wa Fedha wa 2024.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyoondolewa ni mipango ya kutoza asilimia 16 ya ushuru thamani wa ziada VAT kwa mkate, huduma za kifedha na miamala ya fedha za kigeni.

Hata hivyo, Wakenya hasa vijana walifanya maandamano kuwashinikiza wabunge kuukatalia mbali mswada huo wakisema utawakandamiza kwa kuwatoza ushuru zaidi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *