Zimbabwe: Upinzani wamshutumu Mnangagwa kumteua mtoto wake kwenye Baraza la Mawaziri

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameshutumiwa kwa upendeleo baada ya kumteua mwanawe katika baraza jipya la mawaziri kufuatia kuchaguliwa tena kwa uchaguzi wenye utata mwezi uliopita.

Bw. Mnangagwa Jumatatu alimtaja mwanawe, David Kudakwashe, kama naibu waziri wa fedha kama sehemu ya mgawo wa vijana katika bunge.

Pia alimteua mpwa wake, Tongai Mnangagwa kuwa naibu waziri wa utalii, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Mthuli Ncube, mfanyakazi wa zamani wa benki, alibaki kama waziri wa fedha huku mwenyekiti wa kitaifa wa chama tawala cha Zanu-PF Oppah Muchinguri-Kashiri akiteuliwa tena kuwa waziri wa ulinzi.

Mbunge wa chama kikuu cha upinzani cha Citizens Coalition for Change (CCC) Fadzayi Mahere amemshutumu Bw Mnangagwa kwa kuchochea upendeleo.

Hakujawa na majibu rasmi kutoka kwa chama tawala au rais juu ya tuhuma hiyo. Hata hivyo wafuasi wa Bw Mnangagwa wanasema mwanawe amestahili kuwania nafasi hiyo.

Kuchaguliwa tena kwa Bw Mnangagwa kumepingwa na upinzani ukitaja madai ya udanganyifu, huku baadhi ya waangalizi wakisema kuwa kura hiyo haikukidhi viwango vya kikanda na kimataifa.

Share This Article