Ziara ngumu kwa mashetani wekundu Ahly dhidi ya Belouizdad

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri watakabiliwa na kibarua kigumu Ijumaa usiku watakapozuru Algeria, kumenyana na wenyeji CR Belouizdad katika mchuano wa kundi D kuwania kombe la Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Ahly almaarufu Red Devils wanaongoza kundi hilo kwa pointi 5, wakishinda mchuano mmmoja na kutoka sare mbili, wakati Belouizdad wakiwa na pointi 4.

Timu zote ziliambulia sare kappa katika duru ya kwanza jijini Cairo na atakayeshinda mchuano huo wa mzunguko wa nne ataongoza kundi hilo.

Share This Article