Mahakama Kuu imemzuia Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, DPP kuwashtaki wanasiasa wandani wa Naibu Rais Rigathi Gachagua pamoja na wasaidizi wake.
Jaji wa Mahakama hiyo Lawrence Mugambi ametaja kuwa ya dharura kesi hiyo iliyowasilihshwa na mbunge wa zamani wa Nyeri mjini Ngunjiri Wambugu, mbunge wa zamani wa Embakasi West George Theuri na msaidizi wa Gachagua.
Wengine ambao DPP amezuiwa kukamatwa ni wabunge Benjamin Gathiru wa Embakasi Central na James Gakuya wa Embakasi North.
Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga alikuwa amepewa kibalii cha kuwakamata wanasiasa hao na wasaidizi wa Gachagua kwa madai ya kupanga na kufadhili maandamano ya vijana wa Gen Z mwezi Juni 25 mwaka huu kwa lengo la kujaribu kufanya mapinduzi ya serikali.